Dk. Hussein Ali Mwinyi ni mwana wa rais wa zamani Ali Hassan Mwinyi. Baada ya kusoma shule za sekondari za Azania na Tambaza, mwaka 1985 alijiunga na Chuo Kikuu cha Tiba cha Marmara huko Istanbul, Uturuki alipohitimu masomo ya tiba mwaka 1991. Aliongeza masomo kwenye chuo cha kifalme cha tiba katika hospitali ya Hammersmith huko London, Uingereza alipopata shahada za uzamili na uzamivu (PhD) mnamo 1997. Miaka 1993-1995 alifanya kazi ya tabibu kwenye Hospitali ya Muhimbili akaendelea kuwa tabibu na mwalimu kwenye Chuo Kikuu cha Kumbukumbu cha Hubert Kairuki kwenye miaka 1998 - 2000. Mwaka 2020 Mwinyi aliteuliwa na CCM kuwa mgombea wake kwa urais wa Zanzibar akatangazwa mshindi na kuapishwa. Kwa sasa Dk. Hussein Ali Mwinyi ndio Jemedari Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na ndio Mwinyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar..... soma zaidi
Mnamo Tarehe 19, Novemba 2020 Mhe. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi alitangaza Muundo wa Wizara pamoja na Baraza la Mawaziri, ambapo alimteuwa Mheshimiwa Massoud Ali Mohammed (Mwakilishi wa wananchi Jimbo la Ole) kuwa Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ (OR-TMSMIM)..... soma zaidi
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe Simai Mohammed Said, amefanya ziara katika Chuo cha Mafunzo Kilimani(Magereza)
Read More →UAPISHO WA MAKAMANDA WA VIKOSI MAALUM VYA SMZ UAPISHO WA MAKAMANDA WA VIKOSI MAALUM VYA SMZ
Read More →